info@nyumbasaccos.co.tz +255 746 436 049 

Sera hii inatoa mwongozo wa kisheria na uwazi katika uwekezaji wa aina mbalimbali utakaofanywa na chama kwa kuzingatia Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013 na kanuni zake, Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na. 10 ya mwaka 2018 na Kanuni ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2019. Sera hii itatumika wakati wote kama mwongozo wa kuzingatiwa wakati wa kufanya maamuzi ya uwekezaji (Investment decisions) kwa maslahi mapana ya wanachama na chama.