info@nyumbasaccos.co.tz +255 746 436 049 

Sera ya mfuko wa tahadhari unawahusisha wanachama wote wa nyumba SACCOS ambao wanatimiza wajibu wao, kwa kuchangia akiba,kumiliki hisa na kukopa mikopo kutoka kwenye chama.

Sera hii ya mfuko wa tahadhari utazingatia kukinga majanga kwa mwanachama anaposhindwa kurejesha mkopo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, mfuko huu ni tofauti na matengo ya lazima ambayo yapo kwa mujibu wa sheria ya ushirika na mwanachama atakatwa asilimia moja (1%) katika kila mkopo atakaoukopa.