info@nyumbasaccos.co.tz +255 746 436 049 

Sera ya Mikopo ni utaratibu unaoandaliwa kuweka ukomo na uwiano wa kukopesha wanachama kwa kuzingatia Masharti ya chama, Sheria ya vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003, kanuni za mwaka 2004, nyaraka na Maagizo mbalimbali ya Msajili wa vyama vya Ushirika.

Sera hii ya mikopo imeandaliwa kwa ajili ya Nyumba SACCOS ili kuweka wazi taratibu za ukopeshaji Wanachama na vilevile kukidhi matarajio ya wakopaji ambao ni Wanachama waliokusanya nguvu zao pamoja kwa lengo la kupambana na umasikini.

Madhumuni ya Sera ya Mikopo
Kuondoa uwezekano wa kufanya maamuzi bila kufuata utaratibu uliokubalika na itakuwa ni mhimili wa kusimamia shughuli zote za Mikopo.
Kuondoa dhana ya upendeleo baina ya wanachama.

Vyanzo vya Pesa za Mikopo
NYUMBA SACCOS ina vyanzo mbalimbali vya kupata pesa kwa ajali ya kukopesha wanachama wake. vyanzo hivyo ni;- 

  • Akiba za wanachama
  • Faida inayotokana na Mikopo
  • Mauzo ya fomu mbalimbali
  • Adhabu
  • Gharama za mikopo (Loan processing fees)
  • Faida juu ya miradi