info@nyumbasaccos.co.tz +255 746 436 049 

Nyumba SACCOS huandaa mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025. Vile vile, mpango mkakati huu wa miaka mitano umeandaliwa wakati serikali na wananchi kwa ujumla wameelekeza azima,dhamira na nguvu zao katika kuzitumia SACCOS katika kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi.

Mpango mkakati huu wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 unaelezea dira, dhima na maadili ya msingi ya Nyumba SACCOS. Dira ya Nyumba SACCOS ni kuifanya kuwa mtoa huduma za kifedha bora katika Tanzania, wakati dhima yake ni kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi kwa kutoa huduma bora na rahisi kwa wanachama wake.

Utekelezaji wa mpango mkakati umejikita katika kufanikisha maadili ya msingi sita ambayo ni; kumjali mteja, uwajibikaji, ushirikiano, uwazi, uadilifu na weledi.

Mpango mkakati una malengo makuu matano ambayo ni;

  • kuboresha ushawishi na mawasiliano ili kuongeza idadi ya wanachama wa Nyumba SACCOS,
  • kuboresha tija ya wafanyakazi
  • kuboresha ufanisi wa kiutendaji,
  • kuongeza idadi ya wanachama wanaoomba mikopo kwa ajili ya kuwekeza na kuboresha mtaji na uwekezaji toka vyanzo vingine.

Malengo haya matano ndiyo yatakayotoa dira na mwelekeo wa Nyumba SACCOS katika kipindi hiki cha miaka mitano.

Mpango mkakati umelenga kuiboresha/kuibadilisha Nyumba SACCOS na kuwa kiongozi katika utoaji wa huduma bora za kifedha nchini Tanzania. Ili kutimiza malengo yake, Nyumba SACCOS itaelekeza nguvu zake katika kujenga uwezo wa rasilimali watu na kuanzisha mfumo wa upimaji ufanisi ili kuratibu na kusimamia tija ya wafanyakazi wa Nyumba SACCOS.

Kamati ya usimamizi na uongozi wa Nyumba SACCOS wanawajibika katika utekelezaji wa malengo yaliyowekwa katika mpango mkakati. Nyumba SACCOS inaamini kwamba kufanikiwa kwa mpango mkakati kutatokana na kujitolea kwa dhati kwa wanachama wake na uongozi bora.