Nyumba SACCOS Ltd imeanzisha huduma mpya ya mkopo wa ujenzi kwa wanachama wake, ambapo mwanachama ataweza kukopa pesa kwa manunuzi ya vifaa vya ujenzi. Riba itakuwa kiwango cha asilimia 1 kwa mwezi au asilimia 11 kwa mwaka kwa kutumia mfumo wa salio la mkopo linalopungua [Reducing Balance Method]. Kiasi cha mkopo hakitazidi mara tatu [3] ya akiba ya mkopaji. Ulipaji wa mkopo utakuwa kwa kipindi kisichozidi miezi sitini (60).