Mkopo huu hutolewa kwaajili ya Sikukuu na mwanachama atakopeshwa kiasi kisichozidi TZS. 500,000 kwa riba ya 2.08%
Marejesho ya mkopo huu yatakua kwa kipindi cha miezi 6
Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mwingine wa Sikukuu endapo hatakuwa amekamilisha marejesho ya mkopo wa Sikukuu uliotangulia
Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa Sikukuu hata kama ana mkopo mwingine kama vile mkopo wa maendeleo, bila kuathiri vigezo na masharti (1/3 ya mshahara).
Muombaji atahitajika kujaza fomu ya maombi na kuiwasilisha ofisi za Chama