Mkopo huu utatolewa ikiwa mwanachama anahitaji kompyuta. Muda wa urejeshaji ni kipindi kisichozidi miezi 12 Mkopo wa huu utatolewa kwa mkopaji wa kwanza au ikiwa mwanachama aliyekopa amemaliza mkopo wa awali. Kiwango cha juu cha mkopo hakitazidi Shilingi Milioni tatu (Tshs. 3,000,000/=).
Riba itakayotozwa ni asilimia 2.08 kwa mwezi kwa kutumia mfumo wa salio la mkopo linalopungua (Reducing Balance Method). Mwanachama yeyote anaruhusiwa kukopa mkopo huu ili mradi ametimiza miezi 3 inayotakiwa kisheria.