info@nyumbasaccos.co.tz +255 746 436 049 

Mkopo huu utatolewa ili kugharamia Elimu ya mwanachama mwenyewe au familia yake. Muda wa urejeshaji ni kipindi kisichozidi mwaka mmoja (1) Mkopo wa Elimu utatolewa mara mbili kwa mwaka, katika kipindi cha mwezi Julai na Mwezi Januari kila mwaka kwa mwanachama asiye na salio la mkopo wa aina hii.

Kiwango cha juu cha mkopo hakitazidi shilingi milioni tatu (Tshs. 3,000,000/=). Riba itakayotozwa ni asilimia 2.08 kwa mwezi kwa kutumia mfumo wa salio la mkopo linalopungua (Reducing balance method).

Mwanachama atalazimika kuwa na barua/hati ya madai ya ada au gharama nyinginezo kutoka shule au chuo ambayo anatarajia kulipa kwa ajili ya mtoto wake, yeye mwenyewe au mtegemezi wake.