Kiwango cha juu cha mkopo kitakuwa Tshs. Millioni tatu (Tshs. 3,000,000). Marejesho yatakuwa kwa kipindi kisichozidi miezi kumi (12). Kiwango cha riba kitakuwa asilimia 2.08 kwa mwezi kwa kutumia mfumo wa salio la mkopo linalopungua (Reducing Balance Method).
Kiwango cha mkopo kitazingatia ukomo wa mwanachama kukopa unaotokana na akiba na baki ya mkopo wa maendeleo kwa wakati huo. Mkopo wa dharura utatolewa kwa mwanachama ambaye michango na akiba zake zinafikia jumla ya Tsh 500,000 au zaidi.