Mwanachama anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
- Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua kumi na minane (18)
- Awe ni mkazi wa eneo husika.
- Mwenye tabia njema na akili timamu.
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa na anayekubalika kwenye masharti haya.
- Awe amelipa kiingilio, Hisa na kuweka Akiba kwa kiwango kilichopangwa na Mkutano Mkuu na awe anashiriki shughuli za SACCOS.
- Awe tayari kufuata masharti ya chama, Sheria ya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013, kanuni na marekebisho yake.