Hisa za uanachama ni sehemu ya umiliki wa mtaji wa chama ambayo inamilikiwa na mwanachama lakini haitakiwi kuzidi asilimia ishirini ya mtaji hisa wa chama. Hisa zimegawanyika katika makundi yafuatayo:-
Hisa za Lazima
Hisa za lazima ni fedha ambayo mwanachama anaweka chamani ili awe mwanachama kamili pale anapokubali kujiunga na Chama. Idadi ya hisa hizo ni 30 zenye thamani ya Tshs. 750,000/= ambapo gharama ya kila hisa itakuwa Tshs. 25,000/= na ili awe mwanachama atapaswa kununua na kulipia kikamilifu angalau 50% ya hisa na hisa zilizobaki atapaswa kuzilipia katika kipindi cha mwaka mmoja. Mwanachama ambaye atashindwa kutimiza matakwa ya kuwa na Hisa za lazima hataruhusiwa kunufaika na haki za mwanachama katika chama. Viwango vya hisa na akiba vinaweza kubadilishwa kwa maamuzi ya Mkutano Mkuu.
Mwanachama aliyekamilisha kulipia Hisa zote atapewa hati ya kumiliki Hisa.
Hisa za Hiari
Hisa za hiari ni fedha ambayo mwanachama anaweka chamani na anaweza kuichukua wakati wowote anapoihitaji kwa mujibu wa sera. Hisa za Hiari zinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo.
Hisa za Hiari za wanachama zitatunzwa au kuwekezwa katika sehemu salama kama ilivyoelekezwa na sheria, kanuni na sera inayohusika na sehemu kubwa zitawekwa benki.