Dar es Salaam, 18 Agosti 2025 Nyumba SACCOS LTD ilizindua rasmi Mobile Application yake mpya katika Semina ya Wanachama wa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika ukumbi wa NHC House – Samora. Mobile App hii inalenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wanachama kupitia mifumo ya kidigitali kwa urahisi, uwazi na ufanisi. Uzinduzi huo umefanywa na Afisa Ushirika, Ndugu Simkoko, kwa niaba ya Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Angela Nalimi.
Katika hotuba yake, Ndugu Simkoko amesisitiza kuwa hatua ya Nyumba SACCOS LTD kuingia katika teknolojia ya kidigitali ni sehemu ya utekelezaji wa miongozo ya Ushirika za kuhamasisha vyama vya Ushirika kutumia TEHEMA ili kuboresha huduma kwa wanachama, kuongeza uwazi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa.
Kwa upande wake, Menejimenti ya Nyumba SACCOS LTD imeeleza kuwa kupitia Mobile App hii, wanachama wataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo:
- Kuangalia taarifa za akaunti zao za Akiba na Mikopo,
- Kufanya maombi ya Mkopo kwa njia mtandao
- Kupokea taarifa na matangazo ya chama kwa haraka
Aidha, App hii inatarajiwa kupunguza gharama na muda unaotumika na wanachama kufika ofisini, na hivyo kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii ya wanachama.




