nyumba saccos ltd
Nyumba SACCOS Ltd ilianza tarehe 18 mwezi Juni 1969 kwa usajili namba 1904. Chama kilianza na wanachama 103 kama waanzilishi kikiwa na lengo la kuboresha mahitaji ya kiuchumi kwa wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuwawezesha kuweka na kukopa kwa riba ndogo ikilinganishwa na riba zinazotolewa na ma-benki.
DIRA
Kuwa SACCOS kiongozi inayotegemewa katika utoaji wa huduma bora za kifedha nchini.
DHAMIRA
Kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi kwa wanachama wetu kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu na katika mazingara rafiki.
Fanya Maamuzi Sasa
Anza safari yako ya mafanikio na Nyumba SACCOS Ltd wekeza akiba yako na kopa kwa uhuru kwa ustawi wa baadaye.
MIKOPO YETU
Suluhisho linalowezesha ndoto kuwa ukweli kwa wanachama wetu kwa njia rahisi na yenye riba nafuu.
utawala
Nyumba SACCOS Ltd inajivunia uwazi, uwajibikaji, na uadilifu katika uongozi wetu, ukilenga kuwahudumia wanachama wetu kwa
ufanisi na kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
Grace Amini
MenejaRuth Charles
MhasibuDennis Masinda
Afisa TehamaWinfrida Kasonso
Afisa MikopoVeronica Mkumba
Mhudumu wa OfisiHABARI NA MATUKIO
Pata habari za hivi karibuni kuhusu huduma zetu, fursa za uwekezaji, na taarifa muhimu kwa wanachama wetu,
kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi kwa ustawi wao wa kifedha.

November 2, 2024
Mkutano Mkuu 2024
Matukio ya Mkutano Mkuu wa 55 Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 55 ya Nyumba SACCOS Ltd uliofanyika Tarehe 02/11/2024…

October 25, 2024
ZIARA YA KUTOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE
Kujali jamii ni moja ya Misingi 7 ya Ushirika, kwa kulitekeleza hilo Nyumba SACCOS Ltd ilifanya ziara katika Hospitali ya…

April 19, 2024
Huduma za Mikopo na Uwakala wa Fedha
Habari Ndugu wanachama. Tunayo furaha kuwatangazia ya kuwa Huduma za Mikopo na Uwakala wa Fedha mtandao zimeanza kupatikana katika jengo…
WADAU WETU
"Wadau Wetu" wa Nyumba SACCOS Ltd ni nguzo muhimu, wakishirikiana nasi kuboresha huduma,
kujenga ushirikiano thabiti, na kufanikisha malengo ya kifedha